KUAINISHA FURSA ZA LUGHA YA KISWAHILI ZILIZOPO KWENYE MITAALA MIPYA KATIKA SERA ILIYOBORESHWA NCHINI TANZANIA

Bertha Benitho, Dkt. Mussa Omary Amanzi

IKISIRI: Makala hii imejikita katika kuchunguza fursa za lugha ya Kiswahili zilizopo kwenye mitaala mipya katika Sera mpya wa elimu nchini Tanzania iliyoboreshwa. Kwa kuzingatia mabadiliko ya sera mpya ya elimu, Makala haya yamechunguza kwa kina namna Vyuo Vikuu vinavyobuni na kutekeleza mipango ya kimkakati ya kukuza Kiswahili katika mazingira ya kisasa ya elimu. Utafiti huu ulihusisha wataalamu kutoka Vyuo Vikuu vinne. Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) , Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) na Chuo Kikuu Mzumbe(MU). Utafiti ulitumia usampulishaji lengwa kwa kuchagua (wakuu wa idara) na usampulishaji lengwa mpokezano (kwa wahadhiri) kutoka taasisi nne: , kila chuo kikiwa na washiriki watano. Data kutoka kwa wataalamu wa Kiswahili zilikusanywa kwa usaili wa ana kwa ana na uchambuzi wa nyaraka. Uchambuzi wa data ulitumia mkabala wa kimaelezo ili kupata taswira pana na sahihi. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Uamilifu ya Emile Durkheim, inayosisitiza umuhimu wa lugha kama kiungo cha mshikamano wa kijamii na maendeleo ya kitaifa. Matokeo yanaonesha kuwa taasisi za Kiswahili zina mikakati ya kuendeleza lugha hii kwa kuzingatia mabadiliko ya mitaala na matumizi ya TEHAMA, ingawa utekelezaji wake unakabiliwa na changamoto za rasilimali, ushirikiano na ufuatiliaji. Utafiti huu unatoa mwelekeo mpya wa kitaalamu kwa kubainisha nafasi ya Kiswahili katika elimu, biashara na utawala, huku ukitoa mapendekezo ya kisera yatakayowezesha matumizi bora na endelevu ya lugha hii katika maendeleo ya taifa.

Maneno Muhimu; Sera ya Elimu na Mafunzo, Kiswahili, Mitaala, Vyuo Vikuu, Uamilifu wa Kijamii, TEHAMA.

Title: KUAINISHA FURSA ZA LUGHA YA KISWAHILI ZILIZOPO KWENYE MITAALA MIPYA KATIKA SERA ILIYOBORESHWA NCHINI TANZANIA

Author: Bertha Benitho, Dkt. Mussa Omary Amanzi

International Journal of Social Science and Humanities Research 

ISSN 2348-3156 (Print), ISSN 2348-3164 (online)

Vol. 14, Issue 4, October 2026 - December 2026

Page No: 154-165

Research Publish Journals

Website: www.researchpublish.com

Published Date: 20-October-2026

DOI: https://doi.org/10.5281/zenodo.23499480

Vol. 14, Issue 4, October 2026 - December 2026

Citation
Share : Facebook Twitter Linked In

Citation
KUAINISHA FURSA ZA LUGHA YA KISWAHILI ZILIZOPO KWENYE MITAALA MIPYA KATIKA SERA ILIYOBORESHWA NCHINI TANZANIA by Bertha Benitho, Dkt. Mussa Omary Amanzi