IKISIRI: Utafiti huu unahusu kuchambua tija za mwangwi wa falsafa ya Wapare zinazodhihirika katika riwaya ya Kufikirika.Utafiti huu uliongozwa na lengo mahususi moja ambalo ni: Kuchambua Tija za mwangwi wa falsafa ya Wapare zinazodhihirika katika riwaya ya Kufikirika. Kwa kuzingatia lengo la utafiti huu, mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni mbinu ya udodosaji na mbinu ya usomaji maktabani. Kwa kutumia mbinu hizi mbili, data zilichanganuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli yaani, maelezo yalizingatiwa katika uchambuzi wa data. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Elimu Jamii iliyoasisiwa na Hippolyte Taine (1864).Utafiti wa makala haya ulitumia sampuli ya riwaya moja ya Kufikirika na watafitiwa kumi. Utafiti wa makala haya ulitumia Usampulishaji lengwa tajwa mpokezano. Kupitia mkabala wa kitaamuli, uwasilishaji wa matokeo ya utafiti yameonesha kuwa, tija zamwangwi wa falsafa ya Wapare zinazodhihirika katika riwaya ya Kufikirika ni kama ifuatavyo: Husaidia kuponesha maradhi mbalimbali kupitia matumizi ya dawa za asili, husaidia katika ulinzi wa jadi kupitia mazindiko na dawa za asili. Pia, husaidia kudumisha mila na desuri za jamii kupitia utekelezaji wa matambiko na uganga, husaidia kuleta mvua kupitia utekelezaji wa matambiko ya mvua. Vile vile, husaidia jamii kuishi kwa amani na utulivu kupitia masuala ya ugangana matambiko, husaidia kustawisha mazao kupitia utekelezaji wa kafara na matambiko. Husaidia jamii kuishi kwa kuaminiana kupitia viapo na masuala ya uganga, husaidia kudumisha umoja na mshikamano katika jamii kupitia shughuli mbali mbali za kijamii. Pia, husaidia kuleta utawi wa familia kupitia masuala ya ndoa na uzazi, husaidia kuongeza ukoo kupitia falsafa ya familia pana.
Title: Tija za Mwangwi wa Falsafa ya Wapare zinazodhihirika katika Riwaya ya Kufikirika
Author: Rehema Hassan Koshuma, Dkt. Hadija Kutwa Abdallah
International Journal of Social Science and Humanities Research
ISSN 2348-3156 (Print), ISSN 2348-3164 (online)
Vol. 14, Issue 4, October 2026 - December 2026
Page No: 263-273
Research Publish Journals
Website: www.researchpublish.com
Published Date: 24-October-2026